VYANZO vya
uhakika vinadai
Pappy
Tshishimbi
atatua Azam FC
ingawa yeye amefunguka kuhusu usajili mpya akisisitiza kuwa
mipango yake ya usajili haiwezi kuangalia timu moja pekee.
Licha ya hivi karibuni, klabu ya Yanga kueleza kuwa imempa
siku 14 ili kuamua kama ataongeza mkataba mpya au la,
mchezaji huyo raia wa DR Congo, mwenyewe amedai hajaongea na Yanga kuhusu hilo.
Katibu Mkuu wa Yanga, wakili Simon Patrick alisema; “Tulimpa
siku 14, zinakwisha Jumatano ijayo, akija kusaini sawa, la
hatokuja basi maana yake hataki, hivyo tutaachana naye na
kuangalia mambo mengine.”
Habari zinasema kwamba ameanza
mazungumzo ya chinichini na Azam na huenda muda wowote
ikaonekana picha yake amening’iniza uzi wa Azam.
Tshishimbi amekanusha kupewa siku 14.
“Naondoka kurudi
nyumbani likizo, nikiwa huko ndipo nitafanya uamuzi wa timu
gani nijiunge nayo,” alisema mchezaji huyo jana alipokuwa
akizungumza na Mwanaspoti.
chanzo:MwanaSpoti
0 Comments